Dua la mlala hoi,
Angalau apate riziki,
Ya kutosha kumsitiri,
Mpaka keshoye asubuhi.
Dua la mlala hoi,
Angalau mlala hai apite,
Aangushe kipande cha mkate,
Naye lishe apate.
Dua la mlala hoi,
Mwizi apite karibu naye,
Bunda moja lianguke,
Kidogo naye ajienjoy.
Dua la mlala hoi,
Siku moja malaika amlaki,
Ampe naye gari,
Afike mapema kazini.
Dua la mlala hoi,
Kampeni zije haraka,
Mbunge alete pesa,
Hiyo siku ale nyama.
© Reality Check
No comments:
Post a Comment