Chapati

Mzee: Mimi nataka ugali
Mama: Nishapika chapati
Mzee: Sili chapati mimi
Mama: Huna budi
Mzee: Haya basi
Mama: Unataka kufanya nini?
Mzee: Naenda kwa bibi wa pili
Mama: Huyo Ashasafiri
Mzee: haya basi, naenda kwa hoteli
Mama: Chakula cha huko kina nzi
Mzee: Hiki chako kina nini?
Mama: Ladha spesheli
Mzee: Tangu lini chapati kikapata cheti
Mama: Wewe wacha matani
Mzee: Haki ya .... Sili
(Kimya)

Mzee: Mbona ukapika chapati na unajua napenda ugali?
Mama: Chapati ni tamu unazichukia tu kwa sababu hushibi
Mzee: mimi sishibi?
Mama: Una wake wangapi?
Mzee: Si wengi
Mama: Sasa unaona hushibi........
Mzee: Hizo ni njaa tofauti...
Mama: Njaa nayo hustahimili.....
Mzee: Mimi mjasiri
Mama: Wacha woga itisha bakuli
Mzee: Sina njaa mimi
Mama: Tukalale basi
Mzee: Nikiwa na njaa hivi?
Mama: Si nikupakulie chapati?
Mzee: Na cha kitandani vipi?
Mama: Pia huko leo ni chapati
Mzee: Haya basi chapati za kitandani simaindi
(pazia la chumba cha malazi chavutwa)

© Mr. Reality Check.

No comments:

Post a Comment