Ulevi

Chupa ya pombe ifunike,
Ladha ya pombe isiishe,
Ukiitisha nyingine itingishe,
Ukiifungua itoe mvuke.

Ulevi una mawaidha,
Lakini wanyonga fedha,
Ulevi unazo fedheha,
Kama za baba kujikojolea.

Ulevi hauna heshima,
Mtoto hunywa na baba,
Wanatumia meza moja,
Waskie wakitusiana.

Ulevi utamu wa raha,
Ukizidi wakuwa karaha,
Ukijibebea wako kahaba,
Atakupora si haba.

Ulevi si wa madereva,
Isipokuwa wasoskia,
Wale kawaida hufa,
Sisi tutawazika tu!

© Reality Check

No comments:

Post a Comment