Naomba Kukusalimia

Ningependa sana kukusalimia,
Hata kama ni mkono kukupungia,
Angalau nihisi umeniona,
Lakini mimi naogopa,
Vipi utanichukulia.

Labda utaniona kama,
Mmoja wa wajinga,
Wasoweza kutambua,
Salamu si chakula,
Bali ni Ishara,
Ya urafiki na heshima.

Mimi sitaki mapenzi,
Nilitupilia mbali hizo enzi,
Wacha mwingine akuenzi,
Nataka uwe rafiki.

Naomba kukusalimia.

© Mr. Reality Check.

No comments:

Post a Comment